URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY {ulac}

MALENGO MAHUSUSI YA SHIRIKA

i. Kuwezesha jamii kwa kuwajengea uwezo hasa watoto, vijana, wanawake na wazee waweze kuwa na ujasili wa kudai haki zao kwa kuzingatia sheria.

ii. Kuiwezesha jamii kufikia matarajio ya maendeleo endelevu kwa kuzingatia mahitaji halisi ya makundi tete kama vijana, wanawake na wasiojiweza kudai haki kisheria ili waweze kutoka katika lindi la ujinga kwa kuwajengea uwezo na kuwapa ushauri nasaha waweze kufuatilia mambo ya msingi ya kisheria na katiba ya nchi

iii. Kuona jamii yanye afya bora kwa kula vyakula vyenye lishe.

iv. Kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kutunza na kulinda mazingira kwa ajili ya matumizi endelevu ya sasa na ya baadaye.

v. Kufanya utafiti na kutoa ushauri katika nyanja mbali mbali za maendeleo ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.