URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY {ulac}

black and white bed linen

ELIMU YA KISHERIA NA MSAADA WA KISHERIA, MAZINGIRA, LISHE NA AFYA

Providing legal support and education for a brighter future in Urambo.

WELCOME TO

URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY {ULAC}

Empowering Communities Through Legal Support

Urambo Legal Availment and Charity is dedicated to providing legal education, support, and community services for a healthier, informed society.

WASIFU WA SHIRIKA

JINA LA SHIRIKA: URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY

ANUANI NA OFISI: S. L. P 324 URAMBO – TABORA

Makao Makuu ya shirika yapo katika mji wa Urambo na Ofisi za shirika ziko katika jengo la Mzee Kadelege ilipo Zahanati ya Sabato nyuma ya zilipo Ofisi za Tarafa ya Urambo [mkabala na eneo maarufu linalojulikana kwa jina la viwanja vya Mwananchi Square]

AKAUNTI YA SHIRIKA

Shirika la URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY pia lina Akaunti Namba 51310014133 katika Tawi la NMB – Urambo kwa ajili ya kuhifadhi fedha kwa shughuli mbali mbali za shirika/NGO.

HADHI YA SHIRIKA:

URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY ni shirika linaloundwa na watu wa 21 waliopata mafunzo ya wasaidizi wa kisheria kupitia mtaala na kusimamiwa na Chama cha wanasheria Tanzania Bara (TLS) Tanganyika Law Society. Shirika hili lilianzishwa kama kikundi mwaka 10/10/2014 na kutambuliwa na Halmashauri ya Wilaya Urambo tarehe 24/01/2017 kwa jina la Urambo Paralegal Centre kama CBO (Community Based Organization – CBO) kupitia ofisi ya Idara ya Maendeleo ya Jamii na kupewa namba ya utambulisho: (UDC/MJ/2017/00242). Na baadaye tulipotaka kusajili shirika kuwa NGO katika Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, tulipata maelekezo ya kulekebisha katiba na kutafuta jina jingine la shirika lisilo na neno la Paralegal na neno Centre. Malekebisho ya katiba na jina la shirika yalifanywa na wanachama wa shirika na baada ya kukidhi viwango na taratibu za usajili, kisheria shirika lilipata usajili kwa jina la URAMBO LEGAL AVAILMENT AND CHARITY (ULAC) chini ya Sheria ya Usajili wa NGOs Made under section 12 (2) of Act No. 24 of 2002 na kupewa Hati ya Usajili yenye Namba 00009872 ya tarehe 21 Agosti, 2018. Nakala za vyeti zimeambatanishwa.